Matokeo TPL Simba vs Ruvu Shooting leo

Matokeo TPL Simba vs Ruvu Shooting leo

0

Matokeo TPL Simba vs Ruvu Shooting leo

Matokeo kati ya Simba dhidi ya Ruvu Shooting leo 19 March 2019 mechi ikichezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar Es Salaam.

Kipyenga cha Mwamuzi KInapulizwa

Simba 0 – 0 Ruvu Shooting

Mechi Imeanza kwa kasi kiasi huku timu zote zikiwa zimeshafanikiwa kufika langoni kwa mpinzani wake bila mafanikio

Dakika 5

Simba 0- 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 8 Simba wanafanya shambulizi lakini linakosa madhara

Dakika ya 12 Nicolas Gyan anamimina Maji lakini walinzi wa Ruvu Shooting wanasimama imara

Dakika ya 15 Ruvu Shooting wanafanya shambulizi lakini walinzi wa Simba wanasimama imara

Dakika ya 20 Free Kick kuelekea Ruvu Shooting, Inapigwa na Zimbwe Jr inapaa juu ya Lango

Dakika ya 22 Ruvu Shooting wanawakosa Simba bao na kuwa Kona

Dakika ya 24 Simba wanapata kona

Dakika 25

Simba 0- 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 26 Ndemla anaachia shuti kali mpira unakatika

Dakika ya 31 Free Kick kuelekea Ruvu Shooting, Inapigwa na Zimbwe Jr na kuwa kona baada ya beki kucheza kwa Diving Header lakini inakosa madhara.

Dakika ya 33 Kona tena kuelekea Ruvu Shooting, Inakuwa goal kick mara baada ya Mkude kupiga kichwa nje

Dakika ya 33 Emmanuel Martin anajaribu shuti langoni mwa Simba inakuwa nyepesi kwa Dida

Dakika ya 35 Rashid Juma anajaribu kupiga shuti mpira unaenda nje ya Lango

Dakika 40

Simba 0 – 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 43 Wanaingia Meddie Kagere na Haruna Niyonzima wanatoka Rashid Juma na Hassan Dilunga

Haruna kama kawaida baada ya kuingia tu kaanza vitu vyake vya kwenye video kila anapougusa mpira ni burudani

Ruvu Shooting wanafanya shambulizi zuri wanapata kona

HALF TIME

Simba sc 0 – 0 Ruvu Shooting

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha pili Simba wanaanza kwa kasi na wanapata Kona

Goaaaaaaal dakika ya 53 Paul Bukaba anafunga bao kwa Simba

Simba sc 1 – 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 54 Simba wanapata penati baada ya Salamba kuwekwa chini

Goaaaaaal dakika ya 56 Meddie Kagere anaipatia Simba bao la pili kwa mkwaju wa Penati.

Dakika 60

Simba 2 – 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 64 Meddie Kagere anajaribu shuti mpira unamponyoka kipa na kuwa kona

Install App ya Kijanja ya Michezo KWA KUBONYEZA HAPA

Dakika 65 Simba 2 – 0 Ruvu Shooting

Mzamiru Yassin anaingia kuchukua nafasi ya Mo Ibrahim

Dakika ya 82 Fully Zulu Maganga anashindwa kuendelea na Pambano anaonekana kuomba sub mwenyewe

Dakika 2 za Nyongeza

FULL TIME

Simba 2 – 0 Ruvu Shooting

Kwa habari zaidi za Michezo Tufollow Instagram bonyeza hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY