Mbelgiji arekebisha kauli mbiu ya Simba

Mbelgiji arekebisha kauli mbiu ya Simba

0

Simba ikiwa inajiandaa na mchezo wao wa mwisho dhidi ya As Vita, wamekuja na kauli mbiu ‘Do or Die’ kwa lengo la kuongeza motisha kwa wachezaji pamoja mashabiki wa timu hiyo.

Kocha mkuu wa Simba, Partick Aussems ameboresha msemo huo na kuamua kuweka wake wa “Win or Loose’ ‘kushinda au kushindwa’ akisema katika mambo ya mpira hakuna vitu vya kufa.

“Kwenye mpira hakuna mambo ya kufa, lakini kuna kushinda na kupoteza, lakini naamini katika kushinda hasa kwenye mchezo huu wa mwisho,” alisema. Aliongeza kwamba kucheza mechi hii nyumbani kunawaongezea kujiamini tofauti na wakiwa ugenini.

“Tupo nyumbani haitakiwi kuwahofia wageni wetu, wao ndio wanapaswa watuhofie kwa sababu hawapo kwao,” alisema. Simba mpaka hivi sasa ina kauli mbiu mbili, baada ya awali kutumia ‘Yes we Can’ na sasa ‘Do or die’.

source : Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY