Ngassa afichua Siri ya kuvaa jezi namba 16

Ngassa afichua Siri ya kuvaa jezi namba 16

0

Ngassa afichua Siri ya kuvaa jezi namba 16

Winga wa klabu ya Yanga Mrisho Ngassa amefunguka sababu za kwanini alichagua na anavaa jezi namba 16 wakati kuna namba nyingi tu ambazo angeweza kuzivaa.

Mrisho Ngassa ambaye amerejea Yanga baada ya kuondoka kwa misimu kadhaa amefunguka sababu kubwa ni bibi yake ambaye alikaa naye na kumlea kwa muda mrefu.

Ngassa amefunguka kuwa mara nyingi bibi yake alikuwa akimletea vitu alikuwa anaviandika namba 16 na siku aliyokufa bibi yake huyo ilikuwa tarehe 16.

Hata hivyo Ngassa akiwa Mbeya City alikuwa akivaa jezi namba 10, wakati yuko Yanga aliwahi kuvaa jezi namba 17 na akiwa Taifa Stars amewahi kuvaa jezi namba 8.

Lakini akicheza Ndanda Fc , Simba na Azam Fc na kwasasa Yanga mara hizo zote amevaa jezi namba 16.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY