Ngoma aongeza mkataba Azam Fc

Ngoma aongeza mkataba Azam Fc

0


Ngoma aongeza mkataba Azam Fc

MSHAMBULIAJI wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Donald Ngoma, amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Nyota huyo raia wa Zimbabwe, alijiunga Azam FC msimu huu Juni mwaka jana kwa mkataba wa mwaka mmoja uliokuwa unamalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo kwa kusaini kandarasi hiyo mpya ataendelea kubakia hadi Juni 2020.

Ngoma, aliyekosa mechi za mwanzo wa ligi baada ya kuwa majeruhi wa muda mrefu, hadi sasa ni miongoni mwa wafungaji bora wa timu hiyo msimu huu, akiwa amefunga mabao tisa kwenye mashindano yote sawa na Obrey Chirwa, huku akiwa amechangia pasi nne za mabao.

Mpaka sasa ameshiriki kwenye mafanikio ya Azam FC kutwaa taji la Mapinduzi Cup, akiwa amefunga mabao mawili na kutoa pasi moja ya mwisho kwenye michuano hiyo, huku kwenye ligi akiwa amefunga mabao saba.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY