Serengeti Boys wapewa mihela ya kutosha

Serengeti Boys wapewa mihela ya kutosha

0

SERIKALI imetoa Sh bilioni moja kusaidia maandalizi ya timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ‘Serengeti Boys’ pamoja na michuano ya Kombe la Mataifa Afrika ya vijana hao (AfconU17).

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa michuano hiyo itakayofanyika Aprili 14-28, mwaka huu, jijini Dar es Salaam yakishirikisha timu nane.

Akizungumza katika hafla ya kuipongeza timu ya Taifa, Taifa Stars kwa kufuzu michuano ya Afcon 2019 iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, jana, Rais Magufuli alisema awali alikuwa hataki kutoa fedha kusaidia maandalizi hayo, lakini amefurahishwa na ushindi wa Stars na kuaamua kufanya hivyo.

Alisema amekuwa akipigiwa simu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kuhusu suala la kutoa fedha kwa maandalizi hayo, lakini alimwambia hakuna fedha, ila kwa raha aliyoipata baada ya Stars kufuzu Afcon, amekubali kutoa.

Rais Magufuli alisema kingine kilichomshawishi kutoa fedha hizo ni ahadi ya kuwa vijana hao wakishinda michezo miwili, wanapata nafasi ya kushiriki Kombe la Dunia. “Nikimwaga hela (fedha) hapa na nyinyi lazima mkamwage magoli ili kufikia malengo mliyoniahidi,” alisema

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY