Simba: Usajili wa Kwanza dirisha kubwa huu hapa

Simba: Usajili wa Kwanza dirisha kubwa huu hapa

0

Simba: Usajili wa Kwanza dirisha kubwa huu hapa

Hao Simba usiwatanie kabisa wanapotaka chao na kwasasa wamekuwa wako tayari kutoa chochote ili kuhakikisha wanakuwa na kikosi kitakachosumbua katika mashindano ya ndani na nje ya Tanzania yani kitaifa na kimataifa.

Akili ya Simba imekuwa kuchukua wachezaji ambao hawana shaka juu ya uwezo wao wa kusakata kabumbu kwani wamekuwa wakiona faida ya kuwa na kikosi kipana ambacho kimekuwa kikisaidia wachezaji kuwa na Rotation nzuri kiasi cha kuwafanya baadhi yao waweze kupumzika kunapokuwa na mechi za kufuatana.

Siri 4 alizotoa Zahera kuhusu Simba kwa As Vita

Simba pia imekuwa ikipokea ofa nyingi za wachezaji wake kutakiwa na vilabu vikubwa barani Afrika na hata nje ya Afrika kutokana na uwezo waliouonyesha kwenye ligi na hasa michuano ya kimataifa , Wachezaji kama Emmanuel Okwi na Meddie Kagere tayari washakuwa wanakodolewa zaidi macho.

Sasa unaambiwa Simba kwa kuliangalia hilo mapema tayari walishaanza mazungumzo ya kimya kimya na mshambuliaji wa zamani wa Yanga anayekipiga Azam Fc Obrey Chirwa.

Taarifa za kuaminika ambazo kwataunit.co.ke imezipata ni kwamba Obrey Chirwa ameshakataa ofa ya Azam Fc ili kuongeza mkataba na badala yake ameonekana kuvutiwa zaidi na ofa ya Simba ambapo anasubiri msimu uishe amalize kila kitu na Simba ambapo taarifa zinaeleza kuwa Simba wameweka ofa ya milioni 85 kwa Chirwa kusaini miaka miwili.

Kama Obrey Chirwa akasaini Simba huenda huu ndiyo ukawa usajili wa Kwanza wa Simba katika Dirisha kubwa la Ligi litakalofunguliwa baada ya ligi kumalizika wakati wa maandalizi ya msimu mwingine.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY