Siri 4 alizotoa Zahera kuhusu Simba kwa As Vita

Siri 4 alizotoa Zahera kuhusu Simba kwa As Vita

0

UONGOZI wa AS Vita Ulishtuka mapema na kutuma timu ya watu sita kuweka mambo sawa baada ya kumaliza mechi yao ya nyumbani na Al Ahly katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Watu hao wametua nchini tangu wikiendi iliyopita wakati Simba wakiwa bado wapo nchini Algeria walipokwenda kucheza na JS Saoura na tayari wameshaanza harakati zao za kuweka mambo sawa, wakiwatumia Wakongo waliopo hapa nchini akiwemo Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera.

Hata hivyo, wakati Wakongo hao wakitua nchini tangu Jumapili, Simba wenyewe walitua juzi wakitokea nchini Algeria Chanzo cha ndani kinasema kuwa, Zahera alikutana na Wacongo hao juzi na kuwapa siri kadhaa za Simba.

Moja, Zahera aliwaeleza Vita kuhusu kasi ya mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi kuwa anatakiwa kupewa ulinzi muhimu. Pili, aliwaeleza kuwa mashabiki wa Simba wamekuwa wakiipa nguvu kubwa sana timu hiyo na hivyo wawaeleze wachezaji wao wasipaniki.

Tatu, aliwaambia kuwa Simba ni hatari kwenye Uwanja wa Taifa kwani msimu huu haijafungwa mchezo hata mmoja wa ligi na kimataifa, hivyo wanatakiwa kuwa makini.

Ishu ya nne, aliwaeleza kuhusu safu ya ulinzi ya Simba kuwa siyo bora sana kama wapinzani watakuwa na kasi, lakini akiwaonya kuhusu mipira ya krosi kutoka na uwezo wa juu wa mshambuliaji John Bocco na Meddie Kagere.

Hata hivyo, hivi karibuni, Zahera aliliambia Championi kuwa atawapa ushirikiano wa kutosha Vita ili ahakikishe wanaifunga Simba kwa kuwa ni Wakongo wenzake, hivyo habari hii ya chanzo ni uhakika kabisa.

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY