Wachezaji Yanga wapewa dawa kuelekea Mchezo wa Lipuli

Wachezaji Yanga wapewa dawa kuelekea Mchezo wa Lipuli

0

.Uongozi wa Yanga ukishirikiana na kocha wao Mwinyi Zahera wamewapa semina fupi wachezaji yao timu hiyo wakiwapa somo la saikolojia kuelekea mchezo wao ujao dhidi ya Lipuli. Mkutano huo uliofanyika usiku huu katika hoteli ya Nefaland meneja wa hoteli hiyo Winfrida Shonde ndiye aliyeendesha mafunzo hayo ya kisaikolojia kwa wachezaji wa Yanga.

Shonde amesema uwezo ambao wachezaji wa Yanga wamekuwa wakiuonyesha uwanjani umetokana na kuamini kuwa wanaweza kushinda katika mechi zao bila kujali ugumu wa mchezo.

Shonde amesema hata katika mchezo ujao dhidi ya Lipuli utakaopigwa Machi 16 hata kama ukiwa mgumu kama wachezaji hao wataamini wapinzani wao wako sawa kama wao haitakuwa rahisi timu yao kukosa ushindi. Kwa upande wa Zahera amesema siku zote amekuwa akiulizwa juu ya ubora wa timu yake kufanya vizuri licha ya changamoto walizonazo na kwamba ubora wao umetokana na kazi ya kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake.

Naye Kaimu Mwenyekiti wa Yanga, Samuel Lukumay amesema msasa huo wa kisaikolojia waliopewa wachezaji wao una mchango mkubwa kwa wachezaji wao sio wakati huu ambao wanacheza mpira bali hata wakati wakiacha kucheza soka

Mwanaspoti

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY