Zahera awamaliza Lipuli, Mwandila afunguka Hesabu

Zahera awamaliza Lipuli, Mwandila afunguka Hesabu

0

KOCHA Msaidizi wa Yanga Mzambia, Noel Mwandila amesema kuwa hakuna chochote kitakachoharibika kwa timu yake kupata ushindi kwani tayari bosi wake Mwinyi Zahera alikuwa amemaliza maandalizi ya mchezo huo.

Kauli hiyo, aliitoa Mzambia huyo ikiwa ni saa chache kabla ya timu hiyo kuanza safari ya kuelekea Iringa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Lipuli FC utakaopigwa Uwanja wa Samora mkoani huko.

Katika mchezo huo, Mwandila ataiongoza Yanga baada ya Zahera kutimkia kwao DR Congo kwa ajili ya majukumu ya timu ya Taifa ambaye yeye ni kocha msaidizi. Akizungumza nasi, Mwandila alisema kuwa, kabla ya kocha huyo kuondoka alikuwa ameanza programu ya maandalizi ya mchezo huo hivi sasa anamalizia ya hatua ya mwisho kabla ya mchezo huo.

“Tulianza maandalizi ya mchezo wetu huu wa ligi dhidi ya Lipuli baada ya mechi ya KMC tuliyocheza wikiendi iliyopita ambao ulimalizika kwa kuifunga mabao 2-1.

“Maandalizi hayo tuliyaanza wakati kocha wetu Zahera yupo hapa nchini kabla ya kurejea Congo kwa ajili ya majukumu ya Timu ya taifa, hivyo hatuna hofu yoyote ya mchezo huu.

“Na uzuri tulikuwa tulishaanza programu ya mazoezi na mbinu tutakazozitumia katika mchezo huo na hivi sasa tunamalizia tu maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo huo na kikubwa tunahitaji ushindi kama yalivyokuwa malengo yetu,” alisema Mwandila ambaye awali alikuwa kocha wa viungo.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY