Alliance kumbe wameamua iwe vita kweli kwa Simba

Alliance kumbe wameamua iwe vita kweli kwa Simba

0

Alliance kumbe wameamua iwe vita kweli kwa Simba

Kama unafikiri Alliance wamejiandaa kitoto toto kuelekea mchezo dhidi ya Simba basi sahau kabisa juu ya mawazo hayo kwani walichokifanya kuelekea mchezo huo mechi inaweza kuwa ngumu sana kwa Simba.

Kwanza kuelekea mchezo huo kikosi cha Alliance hakikuwa nchini na walisogea nchi jirani ya Kenya kwaajili ya maandalizi ya mchezo huo wa Ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL.

Alliance waliweka kambi ya siku 5 katika mji wa Eldoret uliopo nchini Kenya wakijiandaa na mchezo dhidi ya Simba ambapo siku ya Jumapili usiku ndipo waliporejea jijini Mwanza tayari kwa mchezo huo.

Afisa Habari wa timu ya Alliance Jackson Mwafulango amefunguka kuwa kikosi cha Alliance kiko tayari kwa mchezo huo na wanauhakika Simba hawatachomoa katika mchezo huo kwakuwa wamejiandaa vya kutosha kuhakikisha wanapata Ushindi.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY