Aussems ataja Mchawi mechi ya Kagera

Aussems ataja Mchawi mechi ya Kagera

0

Aussems ataja Mchawi mechi ya Kagera

Simba jana ilijikuta ikiacha alama tatu muhimu katika mji wa Kagera manispaa ya Bukoba ikikubali kichapo kutoka kwa KAGERA Sugar kichapo cha bao 2 kwa 1.

Nyota wa mchezo wa Jana upande wa Kagera alikuwa Ramadhan Kapera “Pires” ambaye aliyetoa pasi ya bao la kwanza baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Simba na kisha kufunga bao la pili la Simba.

Baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Simba Patrick alitaja kitua ambacho aliona kiliwafanya Simba kupoteza MCHEZO huo.

Aussems alisema wamepoteza mchezo huo kutokana na kutocheza vizuri katika kipindi cha Kwanza.

” Shida ilikuwa kipindi cha Kwanza , Niwapongeze kagera walicheza vizuri kipindi cha Kwanza sisi tukacheza vizuri kipindi cha pili sasa huwezi kupata ushindi kwa kucheza vizuri kipindi kimoja tu, Tulipaswa kucheza vizuri vipindi vyote ili kupata ushindi “

Alisema Aussems

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY