Aussems ataja wawili watakaofanya maajabu Lubumbashi

Aussems ataja wawili watakaofanya maajabu Lubumbashi

0

Aussems ataja wawili watakaofanya maajabu Lubumbashi

ZANA Coulibaly na Emmanuel Okwi watafanya kazi kubwa kulazimisha sare yoyote ya mabao na kuwaondoa TP Mazembe kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi hii.

Kocha Patrick Aussems amesisitiza kwamba kikosi chake kitakachocheza wikiendi hii kitakuwa na Sapraizi za kumwaga na Emmanuel Okwi guu lake litafanya maajabu.

“Okwi hatukutaka ajitoneshe katika mchezo huo kutokana na kuwa mechi nyingine ya marudiano tutakayocheza wikiendi hii na kweli tunashukuru alipoingia alionyesha utofauti mkubwa.

“Baada ya kumuona kwenye mazoezi ya siku hizi mbili tuliyoyafanya ni matarajio yangu kumuona akiongeza kitu cha tofauti katika mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Mazembe,” alisema Aussems na kusisitiza kikosi chake kitakuwa na mabadiliko makubwa.

Lakini Zana akasema; “Mashabiki hawatakiwi kuwa na wasiwasi kwa kuwa tunajua tutachoenda kukifanya kwenye mchezo wa marudiano. “Kila timu bado ina nafasi ya kushinda kwa sababu kwenye mchezo wa kwanza hakuna aliyeweza kumfunga mwenzake.”

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY