Aussems atoboa siri nzito za Tp Mazembe

Aussems atoboa siri nzito za Tp Mazembe

0

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems, ametoboa siri ya ushindi wa TP Mazembe juzi kuwa ni uzoefu walionao katika michuano ya kimataifa na rekodi ya mechi 17 waliyonayo.

Aussems alisema ilikuwa ngumu kwao kushinda mbele ya TP Mazembe kutokana na mambo kadhaa ambayo kikosi chake yanakimisi.

Juzi Jumamosi alishuhudia kikosi chake kikitupwa nje ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa na Mazembe mabao 4-1 katika mchezo wa pili wa robo fainali ya kombe hilo.

Aussems Alisemakuwa ilikuwa ni vigumu kwao kushinda mechi hiyo kutokana na kukosa uzoefu wa kimataifa tofauti na ilivyo kwa Mazembe lakini pia rekodi ya wapinzani wao kushindwa kufungwa katika mechi zaidi ya 17 zilizopita katika uwanja wao wa nyumbani.

“Ilikuwa mechi ngumu kwetu, tulipotea baada ya kufunga bao la kwanza tu, tukashindwa kufunga tena.

“Wenzetu kwenye mechi hizi wao ni wakubwa na wana uzoefu zaidi yetu sisi lakini tumejifunza na Watanzania wanatakiwa kujivunia hiki ambacho tumekifanya sisi.

“Unajua isingekuwa rahisi sisi kuwafunga Mazembe tena kwao ambapo wana rekodi kubwa zaidi ya kucheza mechi zaidi ya 17 nyumbani za Ligi ya Mabingwa na hawajapoteza, kitu kikubwa tumejifunza na hiki ambacho tumekipata kitatusaidia kwenye mashindano yajayo,” alimaliza Aussems wakati akifanya mahojiano na gazeti hili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere walipowasili juzi usiku.

Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY