Familia yamuondoa Cannavaro Yanga

Familia yamuondoa Cannavaro Yanga

0

IMEELEZWA kuwa kimya kingi cha Meneja wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kutokuwepo katika kikosi hicho, kinatokana na kukabiliwa na matatizo ya kifamilia. Katika siku za hivi karibuni, Cannavaro amekuwa haonekani kikosini hapo pindi timu hiyo inapokuwa ikicheza mechi zake mbalimbali, huku wengine wakisema amefungashiwa virago.

Championi Ijumaa katika kutaka kupata ukweli wa jambo hilo, lilifuatilia na imeelezwa juu ya matatizo hayo ya kifamilia. “Cannavaro hajafukuzwa isipokuwa ameomba ruhusa ya muda mrefu kuna matatizo yanamkabili, ndiyo maana amekuwa haonekani.

“Bado ana mkataba wa miaka miwili Yanga, hivyo siyo rahisi kukatishia mkataba wake na kama watu wanavyojua klabu haina fedha, hivyo kukatisha mkataba wa mtu ni lazima umlipe, uongozi umekubaliana naye kuhusu maombi yake ya ruhusa, bado ni meneja wa Yanga,” alisema mtoa taarifa.

Championi lilipomtafuta, Ofisa Habari wa Yanga, Dismas Ten kulizungumzia suala hilo alisema suala la Cannavaro ni la kiuongozi zaidi na alipotafutwa mwenyewe beki huyo wa zamani azungumze suala lake, simu yake ilikuwa haipatikani.

source :Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY