Habari mpya kutoka Yanga usiku wa leo 14 April 2019

Habari mpya kutoka Yanga usiku wa leo 14 April 2019

0

Habari mpya kutoka Yanga usiku wa leo 14 April 2019

Baada ya kukusanya Points 6 za uwanja wa CCM Kirumba Yanga ikiutumia uwanja huo kama uwanja wake wa Nyumbani kwenye mchezo dhidi ya African Lyon na Kagera Sugar sasa ni zamu ya Mtibwa Sugar.

Kupitia kwa afisa habari msaidizi wa timu ya Yanga Godlisten Anderson Yanga wamefunguka kuwa kesho Asbuhi kikosi cha Yanga kitaondoka Dar Es Salaam kuelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wake wa ligi kuu dhidi ya Mtibwa Sugar siku ya Jumatano.

Yanga katika mchezo wake dhidi ya Mtibwa Sugar waliibuka na ushindi wa bao 2 kwa 1 ikiwa ndiyo mchezo wa kwanza kwa Yanga na Mtibwa kwenye ligi kuu kwa msimu.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY