Habari njema kutoka Yanga leo 15 April 2019

Habari njema kutoka Yanga leo 15 April 2019

0

Baada ya kugawa vichapo ikicheza katika uwanja wake wa CCM Kirumba ikiutumia kama uwanja wake wa Nyumbani klabu ya Yanga leo asubuhi inaondoka jijini Dar Es Salaam kuelekea mjini Morogoro.

Yanga inaelekea mjini Morogoro kwaajili ya mechi dhidi ya Mtibwa Sugar huku habari njema ikiwa ni kurejea kwa mchezaji wake Ibrahim Ajibu ambaye alikuwa majeruhi na kukosa mechi kadhaa za Ligi kuu na kombe la Shirikisho TFF.

Yanga itafanya mazoezi leo Jumatatu na kesho siku ya Jumanne kabla ya kuwavaa Mtibwa Sugar siku ya Jumatano mechi ikichezwa uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.Install App bora ya Michezo habari zikufikie papo kwa hapo zinapotoka Bonyeza Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY