Kagera Sugar wachekelea kuelekea mechi ya Simba

Kagera Sugar wachekelea kuelekea mechi ya Simba

0

Kagera Sugar wachekelea kuelekea mechi ya Simba

KIKOSI cha Kagera Sugar ya mjini Bukoba kiko kwenye mawindo makali tayari kuikabili Simba, ambayo imekuwa na mwendelezo mzuri wa matokeo katika michezo ya Ligi Kuu Bara, hata hivyo habari njema kwa Wana Nkurunkumbi ni kuanza mazoezi kwa baadhi ya nyota wake ambao walikuwa nje ya uwanja kutokana na majeruhi.

Kagera Sugar ilipoteza michezo yake mitatu mfululizo dhidi ya Azam FC, Singida United na Yanga, kutokana na kuwakosa baadhi ya nyota wake, akiwamo nahodha wa muda mrefu, George Kavilla, mfungaji wao bora msimu huu, Ramadhani Kapera na mshambuliaji, Edward Christopher.

Akizungumza nasi hivi karibuni, Kapera, ambaye amefunga mabao saba, alisema amekuwa nje ya uwanja kwa takribani miezi miwili akikosa mechi 10 na sasa anamshukuru Mungu akiamini mazoezi aliyoanza yatamfanya apangwe katika mchezo dhidi ya Simba.

Alisema licha ya kufunga bao dhidi ya Mtibwa Sugar, alilazimika kucheza mechi hiyo akiwa hajapona vizuri.

“Nimekosa mechi 10 mfululizo na mechi dhidi ya Mtibwa Sugar, nililazimika tu kucheza japo nilikuwa sijapona vizuri kutokana na timu kuwa dhaifu eneo la ushambuliaji,” alisema Kapera.

Mshambuliaji huyo alisema ameanza mazoezi tangu Jumapili na huenda Mexime akalazimika kumchezesha dhidi ya Simba kutokana na hali ya timu yao kwa sasa, japo hajapona asilimia 100.

source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY