Kocha Simba afungashiwa Virago

Kocha Simba afungashiwa Virago

0

Kocha Simba afungashiwa Virago

Klabu ya As Kigali imemfuta kazi kocha wake Irambona Masoud Djuma kufuatia matokeo mabovu ambayo klabu hiyo imeendelea kuambulia.

Kabla ya kutua As Kigali Irambona alikuwa akiinoa Simba Sc ya Tanzania ambapo aligeuka kuwa kocha kipenzi cha mashabiki.

Masoud amefukuzwa kutokana na kuwa na matokeo kuwa mabaya kwa timu hiyo huku katika mechi 5 za mwisho akiwa na As Kigali akipoteza mbili na kutoa sare 3 huku akiwa hana ushindi hata mechi moja.

Masoud aliingia katika kutokuelewana na uongozi wa As Kigali mara baada ya uongozi wa timu hiyo kushindwa kusajili wachezaji waliokuwa akiwahitaji.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY