Masharti 2 aliyotoa meneja wa Tuyisenge kwa Yanga wakitiki ni wao

Masharti 2 aliyotoa meneja wa Tuyisenge kwa Yanga wakitiki ni wao

0

Masharti 2 aliyotoa meneja wa Tuyisenge kwa Yanga wakitiki ni wao

Wakati kocha wa Yanga Zahera Mwinyi akikanusha kuwa hajafanya mazungumzo na mchezaji yoyote kama ambavyo imekuwa ikiandikwa na baadhi ya vyombo vya habari moja ya wachezaji ambao kocha huyo akikanusha Jack Tuyisenge meneja wake amefunguka vingine.

Meneja wa Jack Tuyisenge Patrick Gakumba amefunguka na kukiri kufanya mazungumzo na Yanga kuhusu mchezaji huyo kutua Yanga huku akiwapa Yanga masharti mawili ambayo kama wakiyatekeleza basi Tuyisenge atakuwa mali yao msimu ujao wa ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL.

Kwa Mujibu wa mtandao wa Goal ndugu msomaji wa Kwata Unit ambao ulifanya naye mazungumzo Gakumba amefunguka kuwa

” Nimewapa (Yanga) orodha ya vitu ambavyo wanatakiwa kufanya kabla ya mchezaji wangu hajasaini kwao, Niliongea nao wiki iliyopita kwa kirefu na wameonyesha uhitaji mkubwa wa mchezaji wangu baada ya kuwashawishi msimu huu “

Nimewapa Masharti mawili , Moja ni lazima wahakikishe anapata mshahara wa kila mwezi kwa wakati, lakini pia kuwa na mpango mzuri wa kuhakikisha kiwango chake hakishuki, Ninauhakika kama Yanga watafanya haya basi Tuyisenge atasaini kwao. alisema Gakumba ambaye pia ni meneja wa mchezaji Meddie Kagere wa Simba. Kuzipata tetesi za Usajili kila wakati Install App bora ya Michezo iliyodownlodiwa na watu zaidi ya 10,000 BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY