Matokeo Rs Berkane vs Gor Mahia

Matokeo Rs Berkane vs Gor Mahia

0

Matokeo Rs Berkane vs Gor Mahia

Jana timu ya Gor Mahia ilikuwa dimbani huko mjini Morocco kucheza na timu ya Rs Berkane.

Mpaka saa tatu kabla ya mchezo huo baadhi ya wachezaji wa Gor Mahia walikuwa bado hawajafika uwanjani kwaajili ya mchezo huo na wachezaji nane pekee ndiyo walikuwa tayari kwa ajili ya mechi.

Hiyo msomaji wa Kwata unit ilitokana na usafiri wa kuunga unga waliyotumia Gor Mahia mbaya zaidi wachezaji wakionekana kulala kwenye Floor za Airport wakati wakisubiri kuunganisha ndege hali hiyo ikitokana na viongozi kusema hawana hela ya kuwapeleka wachezaji angalau wakalale kusubiria kuunganisha ndege.

Na hata kundi hilo la pili lilipofika Morocco iliwabidi watumie usafiri wa basi kwa saa 7 mpaka kufika eneo la mchezo huo ambapo walifika na kujumuika na wenzao dakika chache kabla ya mchezo huo.

Katika mchezo huo Gor Mahia walijikuta wakichezea kichapo cha Goli 5 kwa 1 na kufanya matokeo ya jumla kuwa goli 7 kwa 1 na kufurushwa nje ya michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Hakikisha unaInstall app bora ya Michezo kwa sasa BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY