Mo Aficha usajili Nyota Yanga

Mo Aficha usajili Nyota Yanga

0

IMEFAHAMIKA kuwa Yanga tayari ina listi ya wachezaji inaowataka kuwasajili kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara, lakini wameficha listi ya majina huku mwekezaji bilionea, Mohamed Dewji ‘Mo’ akitajwa.

Yanga hivi sasa ipo kwenye kam­peni ya kuhamasisha michango kwa mashabiki wake kwa lengo la kukamili­sha Sh bilioni 1.5 watakazozitumia kwa ajili ya usajili kwenye msimu ujao.

Tayari yapo baadhi ya majina ya­nayotajwa kuwaniwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao wa ligi akiwemo beki, Litombo Bangala anayeichezea timu ya taifa ya DR Congo na Klabu ya AS Vita pamoja na mshambuliaji wa Gor Mahia ya nchini Kenya, Jaques Tuyisenge anayetajwa kuwemo kwenye rada za Mo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazoTumezipata Kocha Mkuu wa Yanga, Mkongomani, Mwinyi Zahera tayari anayo majina ya wache­zaji wazawa na profesheno anaotaka kuwasajili katika msimu ujao ambayo yanafanywa siri kati yake na viongozi.

Mtoa taarifa huyo alisema, hivi sasa wanachokifanya ni kuendelea kukusan­ya michango ya fedha na hadi kufikia mapema Mei, mwaka huu watakuwa wameshazipata na haraka watamk­abidhi kocha kwa ajili ya kuwasainisha mikataba.

Aliongeza kuwa, wanafanya hivyo kwa hofu ya watani wao Simba kuwawahi wachezaji kuwasajili kutokana na jeuri waliyonayo ya mwekezaji wao, Mo.

“Lipo wazi watani wetu Simba hivi sasa wana fedha, hivyo wana jeuri na uwezo wa kumsajili mchezaji yeyote watakayemuhitaji, hivyo kama viongozi kwa kushirikiana na kocha tumepanga kufanya usajili wetu kimyakimya.

“Kikubwa hatutaki kuingia kwenye vita kubwa ya usajili ya Simba, hivyo tulivyokubaliana usajili wetu utaju­likana kwa wachezaji tunaowahitaji pale tutakapokamilisha malengo yetu ya fedha tulizopanga kuzikusanya ambazo ni bilioni 1.5.

“Baada ya kuzipata fedha hizo zitaka­zotokana na michango ya mashabiki, basi haraka tutafanya usajili kwani tayari kocha ana majina ya wachezaji anaowahitaji na kikubwa fedha ndiyo zimekwamisha, hivyo tunaamini kabla ya kocha kwenda kwenye Afon mwezi Juni, mwaka huu tutakuwa tushampa­tia na kufanya usajili,” alisema mtoa taarifa huyo.

Zahera alilithibitisha hilo kuwa kuse­ma: “Ni kweli nina majina ya wachezaji wa hapa nchini wazawa na wengine wa kimataifa kutoka Mali, Nigeria, Ghana na Congo ambao ni wa bei ya kawaida wanaotaka kuja kucheza Yanga.

“Ngumu kuwataja wachezaji hao, kama unavyofahamu hivi sasa viongo­zi wanakusanya fedha zitakazotokana na michango ya mashabiki, kikubwa niendelee kuwahamasisha mashabiki wa Yanga kuendelea kuichangia timu yao ili msimu ujao tuwe na timu bora itakayoleta ushindani.”

source : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY