Msikie alichosema Tshishimbi kuhusu Kutua Simba

Msikie alichosema Tshishimbi kuhusu Kutua Simba

0

Msikie alichosema Tshishimbi kuhusu Kutua Simba

Katika wachezaji ambao wamekuwa wakitajwa kutua Simba msimyu ujao basi kiungo wa Yanga Papy Tshishimbi naye amekuwa akitajwa kuwa ni mmoja wao.

Mkataba wa Tshishimbi na Yanga unamalizika mwisho mwa Msimu Huu na imekuwa ikielezwa kuwa Simba wanamuhitaji kwa udi na Uvumba ili kuzidi kuimarisha safu yao ya kiungo.

Lakini mchezaji huyo ameweka msimamo wake na Kusema kuwa tayari ameshaanza mazungumzo na klabu yake ya sasa ya Yanga kuhusu kuongeza mkataba mpya japo bado hawajafikia maamuzi ya mwisho.

Kiungo huyo msomaji wa Kwata unit ameweka wazi kuwa mipango ambayo amekuwa akipewa na kocha Zahera Mwinyi kuhusu Yanga ya msimu ujao unamfanya kufikiria kuongeza mkataba Yanga na hata ikitokea hajasaini Yanga basi ataenda nje ya Tanzania kucheza soka .

Kauli hiyo inakuja na kuondoa kabisa zile tetesi za Tshishimbi kujiunga na Simba japo kwenye soka lolote linaweza kutokea na hasa ukizingatia mkataba wake na Yanga unaelekea kuisha. Kuzipata Tetesi za Usajili Tanzania kila wakati BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY