Ndayiragije aichokoza Simba

Ndayiragije aichokoza Simba

0

KOCHA wa KMC, Etienne Ndayiragije, amesema atatumia udhaifu wa Simba  kupata pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, utakaochezwa Aprili 26, mwaka huu, Uwanja wa Nyamagana, jijini Mwanza.

Akizungumza nasi jana, Ndayiragije alisema anaendelea kujipanga ili kuhakikisha wanaisimamisha Simba katika harakati zao za kutetea ubingwa msimu huu.

Ndayiragije alisema pamoja na Simba kuwa timu kubwa ambayo ipo katika kiwango kizuri, lakini hawapaswi kuwaogopa, wanachohitaji ni matokeo ya ushindi.

Alisema kikubwa ni kuwaandaa vijana wake kisaikolojia, kiushindani na mbinu ili ziweze kuzaa matunda.

“Mpira una matokeo ya ajabu, hasa kutokana na namna inavyokuwa baada ya dakika tisini, nina imani na kikosi changu tutapata matokeo kwa Simba,” alisema Ndayiragije.

KMC wanashika nafasi ya sita katika msimamo wa ligi hiyo, kutokana na pointi 42, baada ya kucheza michezo 31, wakishinda michezo tisa, sare15 na kufungwa saba

source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY