Ramadhan Kabwili naye kutimkia huku baada ya Msimu

Ramadhan Kabwili naye kutimkia huku baada ya Msimu

0

Ramadhan Kabwili naye kutimkia huku baada ya Msimu

WAKATI ligi ikielekea kumalizika msimu huu tayari baadhi ya wachezaji wamekuwa wakitajwa kumendewa na baadhi ya vilabu huku pia baadhi ya Vilabu vikiwa katika mipango ya kuachana na baadhi ya nyota wake ila mwisho wa siku maisha ni lazima yaendelee.

Ramadhan Kabwili ni moja ya wachezaji ambao mikataba yake na Yanga inaelekea kumalizika ndani ya Yanga na baada ya ligi kumalizika msimu huu basi atakuwa amemaliza mkataba ndani ya Yanga.

Matokeo Yote UEFA Champions League 16 April 2019

Taarifa za kuaminika ambazo kwata unit imezipata ni kwamba Kabwili amepata klabu nchini Saudi Arabia katika klabu ya ligi daraja la kwanza ya Al-Adalh FC .

Klabu hiyo inaelezwa kuwa walianza kumfatilia kabwili toka mwaka 2017 walipomuona akiwakilisha Tanzania katika michuano ya AFCON kwa vijana nchini Gabon.

Klabu hiyo si ya juzi kati tu kama ambavyo unaweza kufikiri bali ni klabu ya toka mwaka 1984 ambapo ndiyo mwaka iliyoanzishwa. Na katika nafasi ya msimamo ligi daraja la kwanza ipo nafasi ya tatu. Kwa tetesi za Usajili Tanzania Install App yetu BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY