Simba washindwa kuwazuia Washabiki Mwanza

Simba washindwa kuwazuia Washabiki Mwanza

0

Timu ya Simba imefanya katika Uwanja wa Kirumba Mwanza kujiweka sawa na mechi yake ya kesho Jumanne dhidi ya Alliance FC Makomandoo Simba wameshindwa kuwazuia mashabiki wa timu hiyo kuingia uwanjani kushuhudia matizi ya wachezaji wao.

Licha ya kwamba haikuwa kazi rahisi mashabiki hao kuingia,lakini kutokana na kashkashi walioionyesha mlangoni umewastua makomandoo na kuamua kuwaruhusu kuingia uwanjani kiroho safi.

Simba ambayo ilitinga uwanjani majira ya saa 10:00 kufanya mazoezi yake kwa ajili ya mechi yake ya kesho Jumanne dhidi ya Alliance FC, ilikuwa na ulinzi mkali kuhakikisha hakuna kinachoharibika. Hata hivyo baada ya kuingia uwanjani mashabiki hao walipewa masharti ya kukaa jukwaani, jambo ambalo walilitii bila usumbufu. Simba imeongozwa mazoezi hayo chini ya Kocha wake Mkuu,Patrick Ausems huku mashabiki wakiwa jukwaani wakifuatilia kwa umakini.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY