Takwimu Mechi 11 Azam Fc vs Mbeya City TPL

Takwimu Mechi 11 Azam Fc vs Mbeya City TPL

0

Takwimu Mechi 11 Azam Fc vs Mbeya City TPL

Ligi kuu soka ya Tanzania bara itaendelea jijini Mbeya kwa mchezo mmoja kuchezwa kati ya wenyeji Mbeya City dhidi ya Azam Fc kutoka Jijini Dar Es Salaam.

Mechi hiyo msomaji wa Kwata unit itachezwa katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya Kuanzia majira ya saa kumi kamili alasiri.

Mechi Hiyo itakuwa ni mechi ya 12 kwa timu hizo kukutana katika ligi kuu soka ya Tanzania bara toka msimu wa Mwaka 2013/2014 Mbeya City ilipopanda daraja na kuwa moja kati ya Timu Tishio nchini Tanzania kwa misimu miwili ya Mwanzo.

KATIKA mechi hizo 11 walizokutana msomaji wa Kwata Unit basi Mbeya City amekuwa hana matokeo ya kufurahisha sana anapokutana na Azam Fc katika mechi hizo iwe anacheza katika uwanja wake wa Nyumbani Sokoine na hata katika uwanja wa Nyumbani wa Azam (Azam Complex).

Ukiachana na matokeo ya sare Mbeya City haijawahi kushinda mbele ya Azam Fc uwanja wa Chamazi huku ikikubali kupoteza mara 3 katika uwanja wake wa Nyumbani wa Sokoine na mara 3 katika uwanja wa Azam Fc .

Hivyo basi katika mechi 11 Azam Fc wamefanikiwa kuifunga Mbeya City mara 6 huku Mbeya City akifanikiwa kupata ushindi mara moja pekee katika mechi hizo 11 na matokeo ya sare yakiwa ni mara 4.

Ushindi pekee ambao amewahi kuupata Mbeya City mbele ya Azam Fc ni ule wa February 20 2016 katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya ambapo Mbeya City aliitwanga Azam Fc bao 3 kwa 0.

Leo 14 April 2019 itakuwa ni mechi ya 12 kukutana je nani anaweza kuibuka kuwa mshindi wa mchezo wa Leo? Ungana nasi pia kupitia App yetu ya Michezo, Bonyeza Hapa Kuinstall

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY