Tetesi za usajili Ulaya leo 17 April 2019

Tetesi za usajili Ulaya leo 17 April 2019

0

Rais wa Barcelona Josep Maria Bartomeu anasema kuwa kiungo wa kati wa Brazil Philippe Coutinho ataruhusiwa kuondoka katika klabu hiyo iwapo wanunuzi wake watalipa kitita cha £355m. Manchester United na Chelsea wanadaiwa kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26. (TVE, via Football 365)

Mkufunzi wa Chelsea Maurizio Sarri na mkufunzi wa zamani wa klabu hiyo Antonio Conte wanafikiriwa kuchukua ukufunzi wa klabu ya Roma. (Corriere Dello Sport – in Italian)

Chelsea iko tayari kumpoteza nyota wao na mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, na sasa inataka kumbadilisha na winga wa Lille na Ivory Coast Nicolas Pepe, 23. (Mirror)

Mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane ameitaka klabu hiyo kumuuza winga wa taifa la Wales Gareth Bale hata iwapo watapoteza pesa.. (Independent)

Tottenham inaongoza katika harakati za kumsaini winga wa Fulham ,18, Ryan Sessegnon kufuatia kazi nzuri inayofanywa na mkufunzi Mauricio Pochettino kuwajumuisha wachezaji kinda wa Uingereza. (Sun)

Mkufunzi wa Newcastle Rafael Benitez anataka kumsaini mshambuliaji wa Burnley ,19, Dwight McNeil, pamoja na kiungo wa kati wa Bournemouth Ryan Fraser, 25, na David Brooks, 21. (star)

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amemtaka mshambuliaji wa Brazil,18, Vinicius Junior kwenda Real Madrid badala ya Sadio Mane wakati mibabe hiyo ya Uhispania ilipomtaka mshambuliaji huyo wa Senegal msimu uliopita. (El Chiringuito, via Metro)

Mkopo wa Denis Suarez katika klabu ya Arsenal haujapendeza na kiungo huyo wa Barcelona huenda akaelekea katika klabu ya Napoli kulingana na ajenti wake (Radio Kiss Kiss, via Mirror)

Arsenal ndio wanaopigiwa upatu kumsaini beki wa Barcelona Samuel Umtiti, lakini Manchester United pia wanamsaka mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 25. (TuttoMercato, via Star)

Liverpool ina hamu ya winga wa Bayer Leverkusen raia wa Ujerumani Julian Brandt. (Bild, via Calciomercato)

Rais wa klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness anasema kuwa atamnunua mshambuliaji wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 20 Kylian Mbappe mara moja iwapo mabingwa hao wa Ujerumani wana uwezo wa kumnunua mchezaji huyo wa PSG . (Deutschen Presse-Agentur, via Goal)

Klabu ya Uingereza Wolves wanafikiria kumsaini winga wa Liverpool mwenye umri wa miaka 18 raia wa Ureno Rafael Camacho. (O Jogo, via Mirror)

Klabu ya Ufaransa ya AS Monaco huenda ikamsajili kiungo wa kati wa Ureno Adrien Silva kwa mkataba wa kudumu kutoka kwa Leicester. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 30 amekuwa katika mkopo katika klabu hiyo tangu mwanzo wa mwaka huu. (France Football via Leicester Mercury)

Mtoto wa kiume wa Cristiano Ronaldo alifunga magoli saba katika kipindi cha kwanza cha mechi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 10 na kuilaza Maritimo. (AS)

SOURCE : BBC

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY