Usajili : Simba sasa Sifa baada ya Ajibu wanasajili na huyu toka...

Usajili : Simba sasa Sifa baada ya Ajibu wanasajili na huyu toka Yanga

0

Usajili : Simba sasa Sifa baada ya Ajibu wanasajili na huyu toka Yanga

Unaambiwa kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems ameshaanza kusuka jeshi lake kwaajili ya mSImu ujao wa ligi kuu soka ya Tanzania bara akiwa na mpango wa kuwaongeza nyota kadhaa na kuwatema baadhi ya nyota kwaajili ya kuifanya Simba kuwa na makali ileile kama ilivyokuwa msimu huu.

Simba tayari inaelezwa wameshamalizana na Ibrahim Ajibu kutoka Yanga na kinachosubiriwa ni ligi iishe na waweze kumalizana naye kila kitu ikiwemo kusaini mikataba ya kuitumikia Simba kwani kwasasa inaelezwa amesaini mikataba ya awali tu.

Lakini kumbe jicho la Kocha Patrick Aussems halikuishia kwa Ibrahim Ajibu tu kwa Yanga bali pia beki na mlinzi wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael naye inaelezwa kuwa yupo katika mipango ya kutua Msimbazi msimu ujao.

Gadiel inaelezwa ni pendekezo la Kocha Aussems lengo likiwa ni kumuongezea changamoto Mohammed Hussein kwani Asante Kwasi ameshindwa kumchallenge mchezaji huyo hivyo huenda akaachwa na Simba.

Gadiel Huenda isiwe kazi kubwa sana kuondoka Yanga kwani inaelezwa kuwa mkataba wake na Mabingwa hao wa kihistoria kuwa unaisha mwishoni mwa Msimu huu. Install App bora ya Michezo habari zikufikie papo kwa hapo zinapotoka Bonyeza Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY