USAJILI : Yanga yawaachia msala Simba na Azam kwa mchezaji huyu

USAJILI : Yanga yawaachia msala Simba na Azam kwa mchezaji huyu

0

USAJILI : Yanga yawaachia msala Simba na Azam kwa mchezaji huyu

Ukitaja tu mechi ya Kwanza ya Watani wa Jadi Simba vs Yanga msimu wa 2018/2019 mechi iliyomalizika kwa sare ya bila kufungana huwezi kuliacha kulitaja jina kipa wa Yanga Beno Kakolanya ambaye alionyesha uhodari mkubwa sana akiwa kama kipa wa Yanga katika mchezo huo kiasi cha kuwa gumzo kila kona.

Baadaye kipa huyo aliingia katika hali ya Sintofahamu na klabu yake ya Yanga kutokana na madai aliyokuwa akiwadai ya mshahara na taarifa kuja kuwa amegoma mpaka kocha wake alipowaamuru viongozi kuwa hamtaki tena Beno.

Yanga chini ya Zahera Mwinyi msomaji wa Kwata Unit ilishamkataa Beno lakini bado anamkataba na klabu ya Yanga mpaka sasa akiwa baada ya msimu atakuwa bado anamkataba wa mwaka mmoja.

Zikufikie za chini ya Zulia jekundu kuwa Tayari vilabu vya Simba na Azam vimeingia katika mawindo ya kuhakikisha vinapata saini ya Beno Kakolanya.

Pata tetesi za usajili kila mara Bonyeza Hapa

Azam wanampango wa kumleta Kipa ambaye atachukua nafasi ya Razack Abalora ambaye amekuwa akiigharimu sana timu hiyo kutokana na vitendo vyake visivyo vya kinidhamu kiasi cha kuwa anapewa sana kadi nyekundu lakini pia kuonekana kukosa mtu wa kumchallenge.

Upande wa Simba wao wanataka kipa kwaajili ya kuja kumpa ushindani kipa Aishi Manula ambaye ameonekana anakuwa mzima ni lazima aanze langoni na kukosa mshindani hasa langoni, Taarifa zinaeleza kuwa kama Beno atasajiliwa Simba basi Dida anaweza kuachwa. Kuzipata Tetesi za usajili punde tu zinapotoka Install App yetu BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY