Yanga Raha : Vinatoka vyuma vinaingia Vyuma

Yanga Raha : Vinatoka vyuma vinaingia Vyuma

0

Yanga Raha : Vinatoka vyuma vinaingia Vyuma

Kesho katika uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro kutakuwa na mchezo kati ya wenyeji wa mchezo Mtibwa Sugar ambao watashuka dimbani kucheza na kikosi cha Yanga kilichosafiri jana mpaka Morogoro kujiandaa kwaajili ya mchezo huo.

Yanga itashuka dimbani bila kuwa na vyuma vyake viwili ambao ni Kelvin Yondani na Kiungo fundi Feisal Salum , Kelvin Yondani atakosekana kutokana na kuonyeshwa kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo kati ya Yanga na Kagera Sugar CCM Kirumba.

Huku Feisal Salum ambaye kwake kupata kadi za njano imekuwa jambo la kawaida atakosa mchezo huo kutokana na kuwa na kadi tatu za njano hivyo kulazimika kuukosa mchezo huo.

Kagere Amchimba Mkwara Makambo

Lakini wakati hao wakikosekana msomaji wa Kwata Unit kuna vyuma vingine viwili vitakuwa vikirejea katika kikosi cha Yanga ambapo Kiungo Fundi mwingine Ibrahim Ajibu atakuwa akirejea baada ya kupona maumivu ya Nyonga.

Na Mwingine atakuwa ni Abdallah Shaibu Ninja atakuwa akirejea katika kikosi cha yanga baada ya kukutana na Rungu la kamati ya Nidhamu alitakiwa kuanza kutumika toka mchezo uliopita lakini hakutumika hivyo katika mchezo dhidi ya Mtibwa anaweza kurejea. Install App bora ya Michezo habari zikufikie papo kwa hapo zinapotoka Bonyeza Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY