Yanga wababe wa Mtibwa mechi 11 walipokutana

Yanga wababe wa Mtibwa mechi 11 walipokutana

0

Yanga wababe wa Mtibwa mechi 11 walipokutana

17 April 2019 majira ya saa nane mchana kutakuwa na mechi ya kukata na shoka kati ya Mtibwa Sugar wakata miwa kutoka Manungu Turiani lakini ambao huamia Uwanja wa jamhuri mjini Morogoro wanapocheza na Simba na Yanga watakuwa dimbani kucheza na Yanga mabingwa wa kihistoria wa Ligi kuu Tanzania bara TPL.

Kuelekea mchezo huo Kwata Unit tunakupa Takwimu ya mechi 11 za mwisho kwa Mtibwa Sugar na Yanga kukutana toka msimu wa 2013/2014 mpaka mechi ya Mwisho ambapo timu hizo zimekutana mara 11.

Katika mechi hizo 11 Yanga wanaonekana kufanya vizuri zaidi kuliko Mtibwa katika mechi hizo walizokutana.

Katika mechi 11 Yanga wanafaida zaidi kwa kushinda jumla ya mechi 6 huku Mtibwa Sugar akiwa ameshinda mara 2 pekee na Mechi 3 timu hizo zikitoka sare.

Katika mechi ambazo Mtibwa Sugar iliifunga Yanga ilicheza katika uwanja huohuo wa Jamhuri ambapo 20.9.2014 Mtibwa Ilifanikiwa kuifunga Uanga bao 2 kwa 0.

Na Katika msimu wa Mwaka jana 15 may 2018 Mtibwa Sugar ilipata ushindi mbele ya Yanga uwanja wa Jamhuri kwa bao 1 kwa 0 lakini Msimu huu Yanga ikaikalisha Mtibwa katika mechi ya mkondo wa Kwanza kwa bao 2 kwa 1. Kupata maujanja zaidi ya Kimichezo Install app yetu BONYEZA HAPA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY