Zahera amtuliza Manara

Zahera amtuliza Manara

0

Zahera amtuliza Manara

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amemtaka Mkuu wa Idara ya Mawasiliano ya Simba, Haji Manara aache kumfuatilia kwa kuwa alichokisema yeye Zahera kuhusu Simba kuvuruga ratiba ya Ligi Kuu Bara ni kweli. Zahera ameyasema hayo kutokana na Manara kuendelea kudai kuwa wao Simba hawataki kocha huyo kuendelea kuizungumzia Simba kila mara kwenye mahojiano yake.

Akizungumza nasi Zahera alisema kuwa Manara hana nafasi ya kumzuia kuzungumza ukweli kwa kuwa timu yake (Simba) imekuwa ikihusika kuvuruga ratiba ya ligi kwa makusudi.

“Ninavyoizungumzia Simba na anachokisema yeye ni ukweli au uongo? Ukweli ni kuwa Simba inaweka rekodi ya dunia katika ligi, maana hata maofi sa wa Caf niliwaeleza juu ya ratiba yao (Simba), wakashangaa inakuwaje timu haichezi mechi za ligi hadi zinafikia kumi.

“Ingekuwa ni uongo yeye Manara angekuwa na sheria ya kunisema kama naisema vibaya timu yake, ila kama ninayoyasema ni ya ukweli basi Manara hana sheria ya kusema kuwa mimi ninawasema wao vibaya. “Tatizo hajazoea kuambiwa ukweli, na hiyo ni shida kubwa kwake, hivyo asinitafute ubaya,”alisema Zahera

source : Champion

NO COMMENTS