Zahera amuonea huruma Mbelgiji Simba kisa hiki hapa

Zahera amuonea huruma Mbelgiji Simba kisa hiki hapa

0

BAADA ya Simba kupoteza dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema kuwa anamuonea huruma kocha wa Simba, Patrick Aussems kwa kuwa anatakiwa kutoka jasho kweli kama anataka kutwaa ubingwa msimu huu.

Zahera amefunguka hivyo kutokana na Yanga kuongoza ligi ikiwa na pointi 74, ikifuatiwa na Azam wenye 66 wakati Simba ikiwa katika nafasi ya tatu na pointi zao 60 lakini Simba ikiwa nyuma kwa michezo nane dhidi ya Yanga iliyo kileleni.

Simba juzi imepoteza mchezo wake wa pili katika Ligi Kuu Bara, baada ya kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar. Akizungumza na Championi Jumatatu, Zahera alisema kuwa kwa upande wake bado anamuonea huruma Mbelgiji huyo kwa kuwa ana kazi kubwa ya kufanya ili aweze kuchukua ubingwa kutokana na mechi nyingi za viporo alizonazo.

“Binafsi namuonea huruma kutokana na yeye kusema Yanga haiwezi kubeba ubingwa kwa kile wanachokifanya wao na kimeanza kuwagharimu na kila mmoja anaona.

“Siwezi kufurahia kinachotokea kwa sababu lazima ubingwa kama kweli anautaka basi akubali kutoka jasho na siyo kirahisi kama wanavyotaka wao, ndiyo maana namuonea huruma kwa uhakika anaojipa na bado ana mechi ngumu za kucheza,”

source : GPL

NO COMMENTS