Zahera ataja watakaokosekana dhidi ya Azam Fc

Zahera ataja watakaokosekana dhidi ya Azam Fc

0

Zahera ataja watakaokosekana dhidi ya Azam Fc

Yanga na Azam ni moja ya timu ambazo zimekuwa na upinzani mkubwa kila zinapokutana katika ligi na hata katika michuano mingine wanapokutana.

Utamu wa mechi ijayo ya Azam na Yanga unatokana na timu zote kuwa bado zinawania ubingwa lakini pia kama itashindikana basi nafasi ya pili.

Kuelekea mchezo huo kati ya Yanga dhidi ya Azam Fc kocha mkuu wa Yanga Zahera Mwinyi ameeleza kuwa kikosi chake kitaingia kambini siku ya Jumatano huku wachezaji wote wakiwa tayari kwa mechi hiyo kasoro mchezaji mmoja.

Mchezaji ambaye atakosekana ni Kelvin Yondani ambaye alipewa kadi nyekundu kwenye mchezo kati ya Yanga dhidi ya Kagera Sugar hivyo ndiye mchezaji pekee atakayeikosa Mechi hiyo ya April 29.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY