Aussems aongezewa mkataba Simba

Aussems aongezewa mkataba Simba

0

Kocha wa Simba Patrick Aussems amesaini mkataba mpya wa mwaka mmoja kuendelea kuinoa timu hiyo.

Hatua hiyo ni baada ya kufikia malengo aliyowekewa katika mkataba unaomalizika hivi karibuni ya kuhakikisha timu inatetea ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara na inafika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Taarifa iliyotolewa leo kupitia mitandao ya kijamii ya Simba haijaweka bayana malengo mapya ambayo kocha huyo amepewa. ‘

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY