Ibrahim Ajibu kujiunga Tp Mazembe

Ibrahim Ajibu kujiunga Tp Mazembe

0

Ibrahim Ajibu kujiunga Tp Mazembe

Ligi inaelekea kuisha na kinachofuata itakuwa ni kusukwa kwa vikosi kwa zile timu zitakazokuwa zikiendelea na ligi kuu soka ya Tanzania bara TPL kwa msimu ujao wa 2019/2020.

Kwasasa moja ya vitu ambavyo timu nyingi zinapambana ni kuhakikisha wanawaongezea wachezaji mikataba hasa wale wachezaji ambao bado wanawahitaji kutokana na kuwa na mahitaji nao kwaajili ya msimu ujao wakati huohuo baadhi ya wachezaji wataachwa kutokana na mahitaji kutowahitaji.

Kwa Tetesi za Usajili kila siku Install App yetu

Kwasasa msomaji wa Kwataunit ukilitaja jina la mchezaji Ibrahim Ajibu Migomba basi akili zinakuja kwenye Yanga na Simba hasa kutokana na tetesi nyingi kutaja kuwa mchezaji huyo huenda akatua Simba huku nyingine zikisema ataendelea kusalia Yanga.

Lakini barua imevuja kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha Kuwa TP Mazembe kuwa katika mipango ya kumsajili mchezaji huyo kutoka Yanga ambaye mkataba wake unaisha 30 June 2019.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY