Matokeo Europa : Chelsea vs Frankfurt

Matokeo Europa : Chelsea vs Frankfurt

0

Chelsea wamefanikiwa kutinga Fainali ya Europa mara baada ya kuwatoa Frankfurt katika hatua ya Nusu Fainali ya michuano ya Europa.

Haikuwa rahisi kwani mpaka dakika 90 zinamalizika matokeo yalikuwa 1 kwa 1 na Aggregate pia ikisoma 2 kwa 2.

Kulingana na kanuni za mashindano ilibidi mbungi iongezwe dakika 30 kupata mbabe lakini bado matokeo yalibaki kama ilivyo ndipo changamoto ya Mikwaju ya penati ilipokuja.

Katika penati 5 Chelsea walipata penati 4 huku Frankfurt wakipoteza penati 2 na kupata 3.

Upande wa Chelsea aliyekosa alikuwa ni Cesar Azpilicueta, wakati kwa Frankfurt waliokosa ni Martin Hinteregger na Goncalo Paciencia

Sasa Fainali kama ilivyo kwa UEFA ambapo timu zote za Uingereza zimekutana Fainali hata kwenye Europa Chelsea atacheza fainali na Muingereza mwenzake Arsenal.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY