Matokeo Yanga vs Ruvu Shooting leo

Matokeo Yanga vs Ruvu Shooting leo

0

Matokeo Yanga vs Ruvu Shooting leo

Matokeo ya moja kwa moja kati ya Yanga dhidi ya Ruvu Shooting mechi ikichezwa katika uwanja wa Uhuru jijini Dar Es Salaam.

Mechi Imeanza

Yanga 0 – 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 5 Ruvu Shooting wanafanya shambulizi zito langoni mwa Yanga na Inakuwa kona

Dakika ya 7 Yanga wanapata Kona

William Patrick anaonekana Kuumia na yuko chini akitibiwa baada ya kugongana na mchezaji wa Yanga

Dakika ya 14 mpira wa kurusha kuelekea Ruvu Shooting

Dakika ya 15 Goal kick inapigwa kuelekea Ruvu Shooting

Goaaaaaaaal dakika ya 16 Papy Tshishimbi anaipatia Yanga bao la Kuongoza assist safi ya Deus Kaseke

Yanga 1 – 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 20 Juma Abdul anapiga mpira ambao almanusra ujae langoni

Dakika ya 22 Emmanuel Martin anawajaribu waajiri wake wa zamani anapiga shuti la mbali lakini Kipa Kindoki anaona mpira mapema

Dakika ya 23 Kaseke anakimbia na kupiga V Pass inayokutana na Makambo anapiga na Kupaisha Juu ya Lango

Dakika ya 24 Kelvin Yondani anapewa kadi ya njano na ni free kick kwa Ruvu Shooting ikielekea Yanga

Dakika ya 26 Papy Tshishimbi anafanya mambo makubwa uwanjani na kusababisha Kona, Yanga wanacheza kona

Inachezwa kona lakini wachezaji wa Yanga wanacheza faulo kabla ya kuucheza mpira

Dakika ya 28 Tshishimbi anawekewa mpira mzuri na Makambo lakini anapiga mpira unapaa juu ya Lango

Dakika ya 30 Yanga wanakosa goli la wazi kabisa, Deus Kaseke alipenyeza mpira kwa Makambo, Makambo akaachia Bakora iliyogonga mwamba wa juu na Kisha kukutana na Raphael Daud anayepiga shuti linalopaa juu ya Lango

Dakika 40

Yanga 1 – 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 45 Abdallah Shaibu Ninja anapewa kadi ya njano, Walinzi wote wa Yanga wa kati wanakuwa wameonyeshwa kati za njano

HALF TIME

Yanga 1 – 0 Ruvu Shooting (16′ PAPY Tshishimbi)

KIPINDI CHA PILI

Kipindi cha Pili kimeanza

Zuberi Dabi anatoka anaingia Hamis Mcha Dakika ya 49

Dakika ya 53 Ruvu Shooting wanapata kona wanashindwa kuitumia

Dakika ya 54 Ruvu Shooting wanapata kona wanashindwa kuitumia vyema inazaa kona nyingine

Ibrahim Ajibu anaingia kuchukua nafasi ya Juma Abdul dakika ya 58

Dakika ya 59 Deus Kaseke anaweka pasi ya Upendo kwa Makambo na Makambo anapiga kipa anakuwa kikwazo

Dakika ya 62 Ruvu wanacheza kona inakosa madhara kwa Yanga

Ruvu Shooting kwasasa wanaishambulia zaidi ya Yanga wakiendelea kusaka bao lakini safu ya Ulinzi ya Yanga imekuwa ikifanya kazi yake.

Dakika ya 66 Thaban Kamusoko anaingia kuchukua nafasi ya Raphael Daud

Dakika 70

Yanga 1 – 0 Ruvu Shooting

Dakika ya 75 Tumba Sued anapewa kadi ya njano kwa mchezo usio wa Kiungwana kwa Papy Tshishimbi

Dakika ya 82 Deus Kaseke anatoka anaingia Said Juma Makapu

Dakika ya 88 Ruvu Shooting ni kama wamehamia Langoni mw Yanga wakiwashambulia mara kwa mara

DAKIKA 4 ZA NYONGEZA

Yanga wanalalamika kutopewa penati baada ya Makambo kuwekwa chini

FULL TIME

Yanga 1 – 0 Ruvu Shooting (16′ PAPY Tshishimbi)

Install App ya Kijanja ya Mchezo Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY