Mghana wa Simba mguu mmoja Yanga

Mghana wa Simba mguu mmoja Yanga

0

WAKATI Nicholas Gyan akitajwa kwenda Yanga, meneja wa mchezaji huyo, Juma Ndambile ameweka wazi juu uwezekano wa mchezaji huyo kujiunga na timu hiyo. Gyan ambaye mkataba wake na Simba unaelekea ukingoni, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wataachana na timu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Nyota huyo alisajiliwa na Simba na huu ni msimu wake wa pili ndani ya kikosi hicho na amekuwa hana nafasi kwenye kikosi cha kwanza kwa siku za hivi karibuni. Akizungumza nasi , meneja huyo alisema kuwa kumekuwa na ofa zinakuja lakini kwa sasa wanasubiri maamuzi ya Simba kama watampa mkataba au watamuacha maana bado hawajaweka wazi.

“Ni kweli ofa zipo za Gyn lakini kwa sasa Simba hawajasema kama wanaachana naye au watamuongezea tena mkataba wa kuendelea kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao. “Ofa zimekuwepo ikiwemo hiyo ya Yanga na kuna kipindi Azam na Singida United nao walimhitaji kwa mkopo na sasa hivi kama kweli ataondoka Simba, basi timu atakayokwenda napenda aende akacheze nafasi ya ushambuliaji na siyo beki kama sasa, sababu anapata wakati mgumu.

Kwa Tetesi za Usajili kila siku Install App yetu

“Na sasa Simba hawawezi kusema lolote kwa kuwa tu wako bize na mbio za ubingwa na mambo ya kuhusu wachezaji gani ambao wanaachana nao tunasubiri msimu umalizike lakini tunaamini kama akiachana na Simba basi anaweza kwenda Yanga ingawa mambo ya soka hubadilika muda mchache sana,” alisema meneja.

Kabla hajatua Simba, kiungo huyo alitokea kwenye kikosi cha Ebusua Dwarfs kilichokuwa kikishiriki Ligi Kuu ya Ghana ambapo huku alikuwa akicheza nafasi ya ushambuliaji tofauti na Simba ambapo mara nyingi amekuwa akitumika kama winga au beki wa pembeni.

Kwa Tetesi za Usajili kila siku Install App yetu

credit : Champion

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY