Simba ikiteleza mechi 3 Yanga ikashinda zote Ubingwa unatua Jangwani

Simba ikiteleza mechi 3 Yanga ikashinda zote Ubingwa unatua Jangwani

0

Simba ikiteleza mechi 3 Yanga ikashinda zote Ubingwa unatua Jangwani

Kilichobaki sasa ni hesabu tu baada ya timu zilizopo kwenye mbio za ubingwa kubakiwa na michezo muhimu inayoweza kuamua bingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Timu ya Yanga imecheza mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting na kubakiwa na mechi mbili tu ambazo ikishinda itakuwa na imekusanya alama 6.

Wakati hesabu zikiwa zimekaa vibaya, Mashabiki wa Jangwani waombee kikosi cha Msimbazi kipoteze mechi zake tatu jambo ambalo litawafanya kuwa mkononi na mechi mbili ambazo hata wakishinda watakuwa na jumla ya alama 88 iwapo Yanga watashinda mechi zote wao watakuwa wamefikisha alama 89.

Install App ya Kijanja ya Mchezo Hapa

Hata hivyo, Kocha wa Yanga Mkongomani Mwinyi Zahera ameweka bayana akisema kuhusu mbio za ubingwa hilo halipo ndani ya uwezo wao kwani kuna mechi ambazo walifungwa na wakashindwa kupata pointi tatu si makosa ya timu bali ni kwa mapungufu ya waamuzi ambao walishindwa kuwa sahihi.

“Tumepoteza mechi ambazo tulinyimwa penati za wazi, tulinyimwa magoli ya wazi na kufungwa magoli ambayo mengine hayakuwa sahihi jambo ambalo lilifanya kukosa pointi ambazo muda huu tungekuwa tupo katika mbio za kuwania ubingwa,”

alisema Zahera na kusisitiza wanataka kushinda mechi zao zilizobaki ili kumalizika katika timu za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara msimu huu. MATOKEO ya mechi mbili zilizopita za Simba baada ya kufungwa dhidi ya Kagera Sugar bao 1-0, na kutoka suluhu dhidi ya matajiri wa Ligi Kuu Bara ni kama yamewashtua mashabiki wa timu hiyo kuelekea mwisho wa msimu huku wakiwa na malengo ya kutwaa ubingwa kwa mara ya pili.

Mwanaspoti

Install App ya Kijanja ya Mchezo Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY