Tetesi za usajili Tanzania leo 27 May 2019

Tetesi za usajili Tanzania leo 27 May 2019

0

KIUNGO wa Azam FC , Stephan Kingue raia wa Cameroon ni kama amegomea mkataba mpya ndani ya Azam FC baada ya kukataa kusaini akiwa bado mkataba wake wa awali haujafikia tamati. Siyo huyo tu,Obrey Chirwa nae amezidi kuweka ngumu baada ya kuwataka viongozi wamkaushie kwanza.

Mratibu wa Azam FC, Philip Alando amesema kuwa, hadi sasa kiungo wao huyo bado hajaongeza mkataba wowote ndani ya klabu hiyo kwa kuwa amehitaji asubiriwe hadi msimu utakaopoisha.

“Tayari tumeshawaongeza mikataba baadhi ya wachezaji wetu akiwemo Donald Ngoma, Bruce Kangwa, Yacub Mohamed na Abdallah Kheri lakini wengine akiwemo Chirwa na Kingue wamataka wasifanye mazungumzo ya kuongeza mkataba hadi ligi itakapoisha, hivyo ligi ikiisha ndio tutaanza kufanya nae

“Kingu amekataa kusaini mkataba hadi ligi itakapofikia ukingoni hivyo tunasubiria ligi itakapoisha ndio tuweze kufanya nae mazungumzo.

“Mikataba ya wachezaji wa Azam ni tofauti na timu nyingine kuna wengine wanamaliza kabla ya msimu kuisha ndio maana mwisho wa msimu hawawi wengi wanaomaliza mikataba,” alisema Alando ambaye ni mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY