Tetesi za usajili Yanga leo 20 May 2019

Tetesi za usajili Yanga leo 20 May 2019

0

Tetesi za usajili Yanga leo 20 May 2019

KUNA kila dalii kwamba, endapo straika Heritier Makambo wa Yanga atakamilisha dili lake la kujiunga na  klabu ya Horoya FC ya nchini Guinea, basi mkali mwingine raia wa Ghana ataziba nafasi yake.

Anayetajwa kuziba nafasi hiyo ni Mnamibia anayekipiga katika klabu ya Lusaka Dynamos ya Zambia, Petrus Shitembi, anayetajwa kuwa hatari katika nafasi ya kiungo mshambuliaji.

Kiungo huyo alisajiliwa na Lusaka Dynamos siku chake baada ya Clatous Chama kusajiliwa na Simba ili kuziba pengo lake kutokana na uwezo mkubwa alionao.

Simba walimsajili Chama kutoka klabu hiyo na kwa haraka nao hawakulaza damu, wakamchukua Shitembi ambaye naye ameingia kwenye rada za Yanga.

Kigogo mmoja wa Yanga amefunguka kuwa kiungo huyo ambaye ana uwezo mkubwa wa kutoa pasi za uhakika na kufunga mabao muhimu, ameshaingia kwenye 18 zao na kilichobakia ni kumalizana tu.

Kwa Tetesi za Usajili kila siku Install App yetu

“Ni kweli Makambo ameondoka lakini hiyo haimaanishi kwamba Yanga inakufa. Tumeshaanza harakati za usajili na muda si mrefu tutamalizana na kiungo kutoka Namibia.

“Ni moja ya viungo wazuri na yeye hana tabu yoyote kuja Yanga. Nadhani ataungana na wachezaji wengine ambao tutawasajili kwani dhamira yetu ni kuisuka klabu yetu upya ili msimu unaokuja tuwakate kilimilimi wapinzani wetu,” alisema.

Alisema kiungo huyo ni moja ya wachezaji wanane wa kigeni ambao kocha wao mkuu, Mwinyi Zahera, alidai atawasajili, huku akisema kuna mastraika wengine watatu kutoka nchi tofauti.

 “Wapo pia mastraika watatu tunaendelea na mazungumzo nao, hiyo kazi inafanywa na kocha wetu, nadhani baada ya kuondoka Makambo, tutashusha mashine nyingine hatari zaidi,” alisema.

Kiungo huyo alianza soka katika timu ya Rundu Chiefs ya nchini kwao Namibia kabla ya kwenda Afrika Kusini ambako alijiunga na University Of Pretoria na baadaye kwenda Ghana kuichezea Ashanti Gold kabla ya kurudi tena na kuzichezea Amazulu FC na Stellenbosch FC na baada ya kuondoka Chama akasajiliwa Lusaka Dynamos kuziba pengo lake.

Kwa Tetesi za Usajili kila siku Install App yetu

DIMBA

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY