Tetesi za usajili Yanga leo 25 May 2019

Tetesi za usajili Yanga leo 25 May 2019

0

Tetesi za usajili Yanga leo 25 May 2019

Hiyo Yanga ya Msimu ujao usipime unaambiwa na huenda ikawa tofauti sana na Yanga ya msimu huu hasa kutokana na mipango ambayo imekuwa ikifanywa na uongozi mpya wa Yanga wakishirikiana kwa ukaribu na kocha wa sasa wa Yanga Zahera Mwinyi.

Jana Yanga walifanikiwa kumbakiza mchezaji wao kiungo Papy Tshishimbi ambaye amekuwa na msimu mzuri sana hasa kuelekea msimu kumalizika huku akigeuka kuwa kipenzi cha wana Yanga.

Tshishimbi ameongezewa mkataba wa miaka miwili kabla ya huu wa awali kumalizika ambapo ulikuwa unaisha baada ya ligi kumalizika.

GADIEL MICHAEL ANAFUATA.

Baada ya kumalizana na Papy Tshishimbi basi inaelezwa kuwa uongozi wa Yanga kwasasa umefikia hatua nzuri ya kumalizana na kumuongezea mkataba mpya wa miaka miwili beki wao wa kushoto Gadiel Michael.

Gadiel Michael naye msomaji wa Kwataunit.co.ke amekuwa na msimu mzuri akiwa Yanga akipata nafasi ya kuanza mara kwa mara katika kikosi cha Kwanza lakini mwishoni mwa Msimu alipata majeraha yaliyomuweka nje lakini kwasasa ameanza mazoezi mepesi.

Kwa Tetesi za Usajili kila siku Install App yetu

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY