Usajili : Deal Done inayomhusu Mtanzania

Usajili : Deal Done inayomhusu Mtanzania

0

Usajili : Deal Done inayomhusu Mtanzania
.
Taarifa kutoka nchini Kenya zinaeleza kuwa nyota wa kimataifa wa Tanzania Hamis Abdallah mwezi wa 4 alivunja mkataba na klabu ya Bandari FC ya Kenya na kutimkia klabu ya Orapa FC ya Botswana.
.
Hamisi amejiunga na vigogo hao wa Botswana kama mchezaji huru kwa dau linalokadiriwa kufikia Tsh Milioni 172 pamoja na mshahara wake wa msimu ujao.
.
Taarifa kutoka kwa wakala wake Mr Sengwe raia wa Zimbabwe, alikielezea chanzo chetu kuwa Abdallah amesaini mkataba wa miaka miwili pamoja na kipengele cha mwaka mmoja na klabu hiyo inayoshiriki ligi kuu. Klabu ya Orapa kwa sasa ipo nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.
.
Inasadikika kuwa Abdallah atapokea kiasi kisichopungua milion 6 kwa mwezi ikiwa ni pamoja na bonusi mbalimbali ambapo itafikia milioni 72 kwa mwaka. Hivyo Hamis ataondoka Botswana na milioni 216 katika kipindi cha mkataba wake wa miaka 2(1).
.
Hamis atakwenda kupambana na Mtanzania mwenzake Rashid Mandawa anayekipiga BDF IX.
.
source : Shaffih Dauda

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY