Usajili : Yanga watua kwa kipa wa Taifa Stars

Usajili : Yanga watua kwa kipa wa Taifa Stars

0

KIPA wa timu ya Tanzania Prisons, Aaron Kalambo, amehusishwa na kusajiliwa ndani ya kikosi cha Yanga kuelekea katika usajili wa wachezaji Ligi Kuu Tanzania Bara.

Awali, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Adolph Rishard, alidai anahitaji kusajili golikipa wa ndani ambaye anafanya vizuri.

Kigogo mmoja wa Yanga aliliambia BINGWA kuwa, inaonekana dhahiri kwamba viongozi wanamtaka Karambo.

Alisema bado hawajazungumza naye lakini ndio mchezaji anayetajwatajwa sana katika usajili wa eneo hilo.

“Wachezaji wanaotakiwa ni wengi lakini kwa wa ndani wanaotajwa ni Aron Karambo, Kenny Ali (Singida) pamoja na Farouk Shakiro (Bandari FC) Kenya,” alisema kigogo huyo.

Kalambo ni miongoni mwa makipa wanaofanya vizuri kwenye timu zao na kufanikiwa kuitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Kwa Tetesi za Usajili kila siku Install App yetu

source : Bingwa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY