Wawa arejea Simba

Wawa arejea Simba

0

BEKI kisiki wa Simba Pascal Wawa anarejea Uwanjani wiki ijayo kuwavaa Singida United, mara baaada ya kukaa nje ya Uwanja kwa muda wa mwezi mmoja akiuguza majeraha ya mguu.

Wawa aliumia katika mchezo wa kwanza Simba ikiwa nyumbani dhidi ya TP Mazembe, kwenye mchezo wa ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya robo fainali katika uwanja wa Taifa, Dar.

Wawa ameeleza kuwa aliambiwa na daktari wake akae nje ya Uwanja kwa wiki mbili bila kufanya mazoezi ya aina yoyote kutokana na aina ya majeraha aliyopata.

Akizungumza nasi , Wawa alisema; “Natarajia kurudi Uwanjani wiki ijayo baada ya kukaa nje kwa muda wa mwezi mmoja, nafikiri hilo ni jambo linalowezekana nimeshaanza kufanya mazoezi makali chini ya kocha wa viungo Adel Zrane.”

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY