Yanga wafunguka ukweli Makambo kujiunga na Horoya

Yanga wafunguka ukweli Makambo kujiunga na Horoya

0

Yanga wafunguka ukweli Makambo kujiunga na Horoya

Taarifa za kushtua kwa wapenzi wa Yanga jioni ya leo 16 May 2019 zilikuwa zikitokea Nchini Guinea katika klabu ya Horoya ambayo kupitia mitandao mbalimbali ilionyesha straika wa Yanga Heritier Makambo akisaini na timu hiyo.

Makambo kulingana na taarifa hizo amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia klabu hiyo.

Hata hivyo kwataunit.co.ke inatambua kuwa mchezaji huyo bado anamkataba na Yanga wa mwaka mmoja hivyo ulifatilia kutaka kujua jambo hilo limeendaje na Yanga watapata nini kutokana na usajili huo.

Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Mshindo Msolla amethibitisha ukweli wa Taarifa hiyo na kukiri kuwa Makambo aliondoka na Mwalimu Mwinyi Zahera

Install App ya Kijanja ya Mchezo Hapa

“Ni kweli Makambo aliondoka na Mwalimu Zahera juzi kwa ajili ya kufanya vipimo vya afya, na tulikubaliana akikamilisha vipimo hivo atarudi ili tufanye mazunguzo”

Taarifa nyingine ambazo siyo rasmi lakini kwata Unit imepenyezewa ni kwamba Heritier Makambo amesajiliwa kwa dau la shilingi milioni 230 za Kitanzania.

Install App ya Kijanja ya Mchezo Hapa

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY