Okwi: Sina bifu na Simba

Okwi: Sina bifu na Simba

0

SAHAU kabisa kinachoelezwa mtaani kwamba straika wa Simba,Mganda Emmanuel Okwi amewafungia vioo viongozi wa klabu yake hiyo hasa suala la kuongeza mkataba kwa kitendo cha kukosa tuzo za ndani ya klabu.
Okwi hakubatika kupata tuzo(MO Simba Award) msimu huu tofauti na ilivyokuwa kwa pacha wake wawili kwenye safu ya ushambuliaji, Meddie Kagere aliyetwaa tuzo ya mchezji bora pamoja na John Bocco akitangazwa mshambuliaji bora.


Hata hivyo Mganda huyo amekanusha vikali na kudai ni vitu vya uzushi tu wanataka kumkosanisha na viongozi wake akidai kila kitu kinajulikana walivyokubaliana kabla ya kujiunga na timu ya Taifa ya Uganda.


ìHakuna ukweli wowote nani hajui kama Simba ni nyumbani, naondoka , narudi kitendo cha kutosaini mkataba havihusiani na tuzo ni vitu vya hovyo, viongozi wa juu wanatambua tulichokubaliana hakuna sababu ya kuvieleza,î alisemabla ya tuzo hizo,Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Clesentus Magori aliweka wazi kuwa wamekubaliana na Okwi kama atapata timu nyingine awe huru kusaini kulingana vipaumbele vyake, lakini ikishindikana milango iko wazi kumwaga wino, Msimbazi.


Mkataba wa mfungaji bora huyo msimu wa 2017/18 umefikia tamati mwishoni mwa msimu huu kama ilivyokuwa kwa kina Aishi Manula, Erasro Nyoni na John Bocco ambao wote tayari wamaeongeza mikataba mipya.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY