Tetesi za usajili Simba leo 13 June 2019

Tetesi za usajili Simba leo 13 June 2019

0

SIMBA imebadili gia angani baada ya kuachana na uamuzi wao wa kuwapiga chini Haruna Niyonzima, Emanuel Okwi na James Kotei.

Habari za ndani zinasema kwamba Kocha Patrick Aussems ambaye kwa sasa yupo kwao akila bata, alipendekeza waachwe wachezaji sita wa kigeni hao hapo juu wakiwemo.

Lakini kutokana na mashindano ya Caf kuwa karibu na usajili ukitakiwa mapema viongozi wamemshauri na sasa watapunguza wanne wa kigeni.

Wakigeni watakaopigwa panga kwa sasa ni Asante Kwasi, Nicholas Gyan, Zana Coulibaly na Juuko Murshid.

Habari zinasema Kocha alitaka kuletewa majembe matano mapya ambayo ni imara tayari kwa Ligi ya Mabingwa Afrika na aliwahi hata kuliambia Championi Jumatano kabla hajaondoka nchini.

Miongoni mwa Wachezaji wapya wa kigeni wanaowindwa na Simba ni straika wa Nkana, Walter Bwalya, Juma Balinya wa Polisi ya Uganda na Francis Kahata wa Gormahia.

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY