Zahera ataja kocha anayemtaka Yanga

Zahera ataja kocha anayemtaka Yanga

0

WAKATI mashabiki wa Yanga wakisubiri kwa hamu kuona nani atakuwa msaidizi wa Kocha Mkuu wa timu yao, Mwinyi Zahera, Mkongoman huyo amemtaja anayefaa kuwa chini yake.

Tayari kuna baadhi ya makocha wamekuwa wakitajwa kutua Jangwani kusaidiana na Zahera, akiwamo Mecky Mexime anayeinoa Kagera Sugar.

Watu wa Yanga wamekuwa wakimtamani Mexime kwa muda mrefu, safari hii wakivutiwa naye zaidi baada ya kuitambia Simba kwa kuifunga mechi zote mbili za Ligi Kuu Tanzania Bara, nyumbani na ugenini.

Mbali ya Mexime, mwingine anayetajwa Yanga ni Fred Felix Minziro na Salvatory Edward waliowahi kuichezea timu hiyo kwa mafanikio makubwa.  

Akizungumza na BINGWA jana kutoka DR Congo, Zahera alisema kuwa anahitaki msaidizi mwenye msimamo ambaye itakuwa ni vigumu kuyumbishwa na mchezaji yeyote yule kikosini mwake.

“Ninahitaji msaidizi mwenye msimamo na asiyeyumbishwa, kocha lazima uwe na msimamo, usiyumbishwe na mchezaji yeyote. Huyo ndiye ninayemtaka,” alisisitiza Zahera.

Hata hivyo, Zahera ameshaweka wazi kutokuwa tayari kuwa na msaidizi mzawa, akitaka atoke nje ya Tanzania

NO COMMENTS

LEAVE A REPLY